VIJANA SIO YOTE YALIYOPO DUNIANI YA KUIGWA

0
161

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vijana nchini kujilinda wakati Serikali nayo ikipambana kuwalinda, na kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema hapatakuwa na wa kutumia mambo mazuri ambayo Serikali imeandaa kwa ajili ya Vijana ikiwa Vijana wenyewe wataingia kwenye matumizi ya dawa hizo.

Rais Samia ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza wakati anahitimisha maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani.

“Mlinzi mkubwa wa nafsi yako ni wewe mwenyewe, mlinzi mkubwa wa maendeleo yako…. wa kesho yako bora ni wewe mwenyewe, Serikali tunaweza kutayarisha kila kitu lakini vijana wote wakiwa wakina Inno na wenzie [kutoka kwenye igizo la waraibu wa dawa za kulevya] hatutapata watu wa kutumia tunayoyatayarisha”.

“….niwaombe sana vijana jilindeni sio yote yaliyopo duniani ya kuigwa, igeni mazuri mabaya yaacheni”. Amesema Rais Samia huku akiongeza kwa kusema kuwa

“Jilindeni na Serikali inawatayarishia mazingira ya kuwalinda, pamoja na wito nilioutoa wa wazazi wenzangu kusaidia kulinda vijana wetu lakini kubwa jilindeni wenyewe”.