Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria operesheni uchumi wa kati wametakiwa kuzingatia kiapo chao kwa kutokubali kutumika na watu wasioitakia mema nchi katika uvunjifu wa amani wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu na baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Kauli hiyo ameitoa Mkurugenzi wa Elimu Michezo na Utamaduni wa JKT Kanali George Kazaula wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa cha 821 JKT Burombora kilichopo Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma ambapo jumla ya wahitimu 1001 wamehitimu mafunzo ya awali ya Kijeshi.
Kwa upande wake Mgeni wa mahafali hiyo mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga ameitumia fursa hiyo kuwasisitiza vijana zaidi kuzingatia kiapo chao na kudumisha nidhamu wakati wote wa maisha yao.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 821 JKT Burombora amewakumbusha vijana kutambua kuwa mchango wao ni muhimu katika kudumisha maendeleo ya Taifa kwa kupeleka mafunzo walioyoyapata wenzao ambao hawakupata nafasi ya kushiriki katika mafunzo hayo.