Vifo vya uzazi vyapungua Lindi

0
78

Mkuu wa mkoa wa Lindi , Zainabu Telack amesema, maboresho katika sekta ya afya yanayoendelea kufanyika mkoani humo yamesaidia kupunguza vifo vya akina mama wakati wa uzazi.

Amesema kwa mwaka 2020 kulikua na vifo 54, mwaka 2021 vifo 47 na kuanzia mwezi Januari mwaka huu hadi sasa vimetokea vifo 14 tu.

Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ameyasema hayo alipokuwa akisoma salamu za mkoa huo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

Ameongeza kuwa maboresho katika sekta ya afya yanayoendelea mkoani humo, pia yameuwezesha mkoa huo kuwa na dawa katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za afya, ambapo umepatikanaji wake kwa sasa ni asilimia 86.

Kauli mbiu ya kitaifa ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka huu ni Imarisha Usawa,
na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais Samia Suluhu Hassan.