Vifo viwili vyaongezeka ajali ya Mbeya

0
220

Majeruhi wawili kati ya 22 wa ajali iliyotokea Juni 05, 2024 katika eneo la Mbembela mjini Mbeya ambao walikuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wamefariki dunia na kufanya idadi ya vifo katika ajali hiyo kufikia 16.

Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo Peter Seme amesema waliofariki dunia katika ajali hiyo ni wanaume 13 na wanawake watatu.

Amesema matibabu yanaendelea kwa majeruhi watatu kati ya majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo na kwamba wengine wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu.