Vifo vitatu vyathibitishwa ajali ya Precision

0
327

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amethibitisha kutolewa kwa miili mitatu katika ndege ya Shirika la ndege la Precision Air kufuatia ajali iliyotokea mapema hii leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bukoba, Chalamila amesema majeruhi 26 wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera.

Habari zaidi kutoka mkoani Kagera zinaeleza kuwa, muda wowote kuanzia hivi sasa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili mjini Bukoba kuongoza kazi ya uokoaji.