Vifo ajali ya Mtwara vyaongezeka

0
214

Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dkt. Mohamed Nyembea amethibitisha kuongezeka kwa vifo vya mwanafunzi wawili wa shule ya msingi ya King David, ambao walikuwa miongoni mwa majeruhi watano waliokuwa katika hali mbaya wanaopartiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa huo, Ligula.

Vifo vya wanafunzi hao vinafanya idadi ya vifo kufikia watu 13, ambao ni wanafunzi 11 na wengine wawili ambao ni dereva na msaidizi wake.

Majeruhi watano wamehamishiwa katika hospitali ya Ndanda kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi baada ya hali kuwa mbaya.

Habari zaidi kutoka Mtwara zinaeleza kuwa miili ya wanafunzi hao imeagwa alasiri ya leo katika hospitali ya rufaa ya Ligula.

Watu hao wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi mkoani Mtwara baada ya basi dogo la shule kutumbukia kwenye korongo katika eneo la mteremko la Mjimwema kata ya Magengeni, Mikindani mkoani Mtwara wakati wakielekea shuleni.