Video: Ufanyaji wa ‘scrub’ mara kwa mara unavyoweza kuwa hatari

0
484

Watu mbalimbali hasa katika maeneo ya mijini wamekuwa na utaratibu wa kisafisha nyuso zao (scrubbing) mara kwa mara, jambo ambalo wengi wamesema kuwa huwasaidia kuwa na ngozi nzuri.

Licha ya manufaa mengi ya kusafisha ngozi kwa kutumia viambata vya kemikali na vile vya asili, usafi huo unapofanyika kwa njia isiyo sahihi huweza kusababisha madhara makubwa.

Wataalam wanaelekeza kuwa usafi huo usifanyike mara nyingi sana, na pia unapofanyika, mfanyaji asisugue ngozi kwa nguvu na aepuke kutumbua vipele vilivyopo usoni.

Tumekuandalia taarifa kwa kina kuhusu njia salama za kufanya usafi huo;