Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma amemuapisha Samia Suluhu kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla ya kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan imefanyika Ikulu jijini Dr es salaam na kuhudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali.
Miongoni mwa viongozi hao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya awamu ya Nne Jakaya Kikwete na Aman Abeid Karume ambaye ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo.