Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) kusimamia malengo na misingi ya kuanzishwa kwake, na kukemea vitendo vya udhalilishaji.
Rais Samia ametoa wito huo wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa 10 wa UWT unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
Aidha, ameitaka Jumuiya hiyo kuendelea kukemea tatizo la udhalilishaji kwa wanawake na watoto na kusimamia maadili.
Kupitia mkutano huo wa UWT, Rais Samia amezitaka jumuiya za Chama cha Mapinduzi kuhakikisha zinashirikiana ili kujenga chama imara kitakachosukuma maendeleo ya Taifa.
Katika Mkutano huo mkuu wa 10 wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania, wajumbe wa mkutano huo wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wa juu.
Rais Samia pia amewataka wajumbe wa mkutano huo kufanya uchaguzi kwa amani na kuhakikisha wanavunja makundi mara baada ya uchaguzi na kujenga umoja na mshikamano.