Mchakato wa kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Benjamin Mkapa Stadium (Uwanja wa Benjamin Mkapa) umekamilika.
Kubadilishwa kwa jina la uwanja huo ni moja ya njia za kumuenzi Hayati Benjamin Mkapa, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu.
Akiwa madarakani Hayati Mzee Mkapa alipigania vyema sekta ya michezo nchini na kufanikisha kujenga Uwanja wa Taifa. Baada ya kifo chake yaliibuka maoni kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali kuhusu uwezekano wa kubadili jina la uwanja huo na kwa kuwa lilikuwa wazo zuri, Rais Dkt. John Magufuli aliafiki na shughuli ya kubadili jina ikaanza mara moja.