Uteuzi wa Profesa Manya ni sahihi : Waziri Mkuu

0
195

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dkt John Magufuli kumteua Profesa Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini ni sahihi.

Amesema kuwa mchango wa Profesa Manya kwenye sekta ya Madini ni mkubwa na unajulikana, hivyo anaamini kitendo cha kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Madini kitasaidia kuinua sekta ya Madini nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kuapishwa kwa Profesa Manya kushika wadhifa huo wa Naibu Waziri wa Madini.