Uteuzi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani

0
297

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Waziri Masauni amemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Jumanne Sagini kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Wakati huo huo, Waziri Masauni amemteua Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Aidha Waziri Masauni amewateua Wajumbe wa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha.

Wajumbe wengine ni pamoja na:-

  1. Dkt. Henry Swai
  2. Ponziano Lukosi
  3. Rogatus Matavila
  4. Mhandisi Victor Seff
  5. Rtd DCP Mohamed Mpinga
  6. Neema Swai
  7. SACP Johansen Kahatano
  8. Dkt. Baghayo Saqware
  9. Mhandisi Yona Africa
  10. Isabela Nchimbi
  11. Agustas Fungo
  12. Faraji Abri
  13. Issa Nkya
  14. Dorice Mutalemwa
  15. Abdallah Miraji
  16. Mhandisi Dkt. Phil Makini
  17. Anord Mtewele

Uteuzi huo umeanza tarehe 01 Septemba, 2022