Uteuzi mpya wa Naibu Waziri wa Madini

0
219

Rais John Magufuli amemteua Profesa Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Profesa Manya pia ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania.

Uteuzi wa Profesa Manya unaanza leo Disemba 11 na ataapishwa leo mchana Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.