UTABIRI: Mikoa inayotarajiwa kukumbwa na mvua kubwa

0
385

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa leo Ijumaa, Januari 17, katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara.

Katika taarifa iliyotolewa Januari 16, TMA imesema kuwa mvua hizo zinaweza kuambatana na upepo mkali katika maeneo hayo.

Athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo ni pamoja na kuharibu makazi ya watu hasa kwa watu wanaoishi maeneo hatarishi kama vile mabondeni, au karibu na mikondo ya maji.

Ucheleweshwaji wa usafiri na baadhi ya shughuli za kiuchumi
na kijamii kusitishwa.

Pamoja na tahadhari hiyo ya mvua, TMA imetahadharisha juu ya upepo mkali katika ukanda wa bahari ya pwani.

Upepo huo utaanza Jumamosi, Januari 18 hadi Januari 21, hivyo imewataka watumiaji wa vyombo vya baharini na umma kwa ujumla kuchukua tahadhari.