USAID kusaidia kupatikana Megawati elfu 30 Afrika

0
160

Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia mradi wake wa ubia wa nishati ya umeme wa Power Africa, linalenga kuongeza Megawati elfu 30 za umeme Barani Afrika, ili kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika majumbani na kwenye maeneo ya biashara ifikapo mwaka 2030.

Kauli hiyo imetolewa jijini Washngton DC nchini Marekani na Mshauri Mkuu wa mradi huo Michael Jordan ambaye amesema lengo la kuongeza Megawafi hizo ni kusaidia Afrika kuondokana na changamoto ya nishati ya umeme ambayo itasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa watu wake.

Amesema kwa sasa Power Africa inaendelea kutafuta fedha kupitia washirika mbalimbali ikiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo Afrika na nchi za Umoja wa Ulaya ili kuwezesha azma ya kuzisaidia Serikali za Afrika kunufaika na Megawati hizo elfu 30 za umeme ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake msimamizi wa shirika la USAID Idara ya Afrika Janean Davis amesema, Marekani itaendelea kuisaidia Afrika kupitia miradi ya ubia inayolenga kubadilisha maisha ya watu kiuchumi.

Mradi wa Power Africa ulianzishwa mwaka 2013 ambapo Tanzanaia ni miongoni mwa nchi ambazo zimenufaika kupitia mradi huo.