Upete na D’jaro wazawadiwa pikipiki

0
179

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limetoa zawadi za pikipiki kwa watumishi wawili wa shirika hilo, D’jaro Arungu na Nazareth Upete ikiwa ni ishara ya kutambua uchapakazi wao.

Akifafanua juu ya kazi walizofanya watumishi hao ambazo zimepelekea kupewa zawadi hizo, Mkurugenzi wa Huduma za Redio, Aisha Dachi amesema D’jaro ameonesha umahiri katika kazi ya utangazaji ambapo alitunukiwa tuzo ya Mtangazaji Bora wa Kiume kwa Afrika, huku Upete akipokea sifa nyingi kutokana na kipaji chake cha utangazaji mpira kilichoonekana zaidi msimu wa Kombe la Dunia.

Akikabidhi zawadi hizo ambazo zimepokelewa na wawakilishi wa watumishi hao, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mathew Kundo amesema TBC imefanikiwa kuibua vijana wenye vipaji na ubunifu hata kulifanya shirika kuwa mahiri katika kazi zake.

Aidha, Kundo amezindua rasmi baraza jipya la wafanyakazi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jijini Dar es Salaam.