Ulega : Changamkieni fursa kwenye ufugaji

0
154

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaoishi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Iringa na Njombe kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya mifugo hasa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Waziri Ulega ametoa wito huo mkoani Iringa wakati akihitimisha mashindano ya kumi ya kuhifadhi Qur’an Nyanda za Juu Kusini yaliyoandaliwa na taasisi ya Dhi Nureyn.”

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo mahususi katika wizara yangu ya kuhakikisha sekta ya mifugo inainuka na kusaidia Watanzania kupitia fursa mbalimbali ambazo yeye ameendelea kuzitoa katika sekta hiyo.” Amesema waziri Ulega