Ukune yapata gari la Wagonjwa

0
188

Wananchi wa Kata ya Ukune katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, wameishukuru Serikali kwa kuwapatia gari la kubebea wagonjwa.

Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi hao mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Fabiani James na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kahama Theresphora Saria wamesema gari hilo litasaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto na kwamba awali walikuwa wanalazimika kutumia usafiri wa pikipiki kuwasafirisha wagonjwa kwenda kwenye Hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ukune Dkt.Elikana Lubango,amesema gari hilo litatumika kubeba wagonjwa wakati wote litakapohitajika huku Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani akisema Serikali imetoa magari hayo ukiwa ni mpango wa kuwaondolea wananchi adha ya kuwasafirisha wagonjwa kwenda kupata matibabu kwenye Hospitali kubwa.