Apelo Apeto (32) ni raia wa Togo na ni miongomi mwa watu waliokuwemo katika ajali iliyotokea Februari 25. 2024 katika eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha
na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.
Kwa sasa Apelo anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, Mount Meru ambapo
ameishukuru Serikali kwa huduma nzuri za matibabu anazopatiwa hospitalini hapo.
Amesema kwa namna ajali hiyo ilivyokuwa na huduma alizopatiwa kama asingekuwa Tanzania angekuwa amekwishafariki dunia na kwamba ukarimu wa Watanzania ndio uliookoa maisha yake.
“Kwa ajali hii ningekuwa nchini kwetu tayari ningekuwa nimepoteza maisha, kwani kule bila kulipia huduma za matibabu hupatiwi huduma, lakini kwa Tanzania walivyo wakarimu na weledi wameweza kuokoa maisha yangu mpaka sasa naendelea vizuri na naweza kuongea,” Amesema raia huyo wa Togo
Apelo alikuja Tanzania kushiriki kwenye semina iliyokuwa ikifanyika mkoani Arusha, ambapo pia walikwenda kufanya utalii na walipokuwa wakirejea ndipo wakapata ajali.