Ukarabati wa Kivuko cha MV. Magogoni unatarajiwa kukamilika Desemba, 2024 na kurejeshwa nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile aliyetaka kujua ni lini matengenezo ya MV. Magogoni yatakamilika na kivuko hicho kurejeshwa nchini ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.
Mwezi Februari, 2023 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ilisaini mkataba wa ukarabati wa MV. Magogoni wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5.
Kasekenya amesema lengo la ukarabati huo ni kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini, kuharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine.