Ukaguzi wa Vituo

0
216

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akikagua baadhi ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, lililoanza Februari 14 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku saba, ambapo vituo vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.