Ujenzi mnada wa Pugu wakabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa

0
106

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, amesema atahakikisha kazi ya ujenzi wa eneo la mnada wa mifugo wa Pugu inakamilika kwa wakati ili mnada huo uendane na mahitaji ya mifugo katika mkoa huo.

Makalla amesema, kutokana na mahitaji ya mifugo na uwepo wa machinjio ya kisasa ya mifugo Vingunguti, lazima kazi ya ujenzi wa maeneo ya mnada huo imalizike ili kupata mifugo iliyo bora Zaidi.

“Dar es Salaam kwa sasa ndio lango kuu la biashara sasa ni lazima na biashara ya mifugo iwe na ubora unaohitajika na kwa kuanzia tutahakikisha kazi ya ujenzi wa mnada wa Pugu inakamalika kwa wakati”-Amesema Mkuu wa Mkoa.

Makalla amesema, uwepo wa ndege za kisasa za Tanzania unaongeza mahitaji ya nyama za mifugo kutoka Tanzania na hivyo ni jukumu la Serikali ya mkoa pamoja na wizara ya Mifugo kusimamia ujenzi wa mnada huo.