Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga, ameshiriki ujenzi wa kituo cha afya eneo la Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga.
Hadi kukamilika kwake, ujenzi wa kituo hicho cha afya utagharimu shilingi milioni 250, fedha zitokanazo na tozo za miamala ya simu.
Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya eneo la Sindeni kutawasaidia wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakitembea umbali wa kilomita 39 kufuata huduma za afya.
Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah anaendelea na ziara yake mkoani Tanga.