Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanza ujenzi wa barabara ya Visiga – Zegereni- Misugusugu iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani, yenye urefu wa kilomita 12.5 kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kuwezesha malighafi kuingia viwandani kwa urahisi, lakini pia kutoa bidhaa viwandani na kupeleka sokoni.
Akizungumza mkoani Pwani wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Bodi ya Ushauri ya TARURA mkoani humo, Meneja wa wakala huo wilaya ya Kibaha Mhandisi Samwel Ndoveni amesema, mradi huo wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unalenga kuhakikisha viwanda vilivyo katika maeneo hayo vinafikika kwa urahisi kipindi chote cha mwaka.
Barabara hiyo ya Visiga – Zegereni – Misugusugu inajengwa
kwa uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa zaidi ya tani 30.