Uganda yatambua mchango wa TPDC

0
182

Serikali ya Uganda kupitia mamlaka ya uwekezaji nchini humo imetoa tuzo ya heshima kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutokana na mchango wake wa kufikia maamuzi kwenye uwekezaji mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Tuzo hiyo imekabidhiwa mkoani Dar es Salaam kwa TPDC na Bryan kutoka kwenye mradi huo, ambaye amesema mchango wa kitaalam wa shirika hilo katika kufanikisha utekelezaji wa
mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki ni mkubwa.

Amesema mradi huo umepitia hatua kadhaa za maamuzi ambayo yalifanyika kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo sheria na sera za uwekezaji pamoja na uzoefu wa nchi na taasisi zake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio amesema ameipokea ruzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania wote.

Ameahidi shirika hilo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kufanikisha kuanza kwa mradi huo mkubwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki.
wenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni nane kutoka Tanga, Tanzania hadi Hoima, Uganda.