Ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi wa AU

0
293

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo Februari 5, 2022 akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo “Kuimarisha Lishe na Usalama wa Chakula barani Afrika: Kuongeza kasi ya Uzalishaji katika Kilimo,Maendeleo ya Rasilimali Watu na Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi na Kijamii.”