Ufaulu kidato cha nne waongezeka kwa 0.49%

0
171

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2022, ambapo watahiniwa wa shule 456,975 kati 520,558 ambao ni sawa na asilimia 87.79 wamefaulu.

Watahiniwa hao wamefaulu kwa kupata madaraja kuanzia la kwanza, daraja la pili, daraja la tatu na daraja la nne.

Kwa mujibu wa NECTA, kati yao wasichana ni 243,285 na wavulana ni 213,690.

Ufaulu wa watahiniwa wa shule kwa kidato cha nne mwaka 2022 umeongezeka kwa asilimia 0.49 ikilinganishwa na mwaka 2021.