Shirika la Fedha Duniani (IMF) linasema vita nchini Ukraine vimesababisha uchumi wa dunia kuporomoka katika kipindi kifupi kuliko ambavyo ilikuwa ikitarajiwa. na hali hiyo inatarajiwa kuongezeka.
Takwimu zilizotolewa na IMF zinasema uchumi huo umeporomoka kutoka asilimia 6.1 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 3.6 ya ukuaji wake wa kawaida mwaka huu.
Bei za bidhaa katika mataifa mbalimbali duniani zimeendelea kupanda yakiwemo mafuta tangu Russia ilipoivamia Ukraine kijeshi, huku mashirika kadhaa ya kimataifa yakitahadharisha kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali.
Mashirika hayo yamesema nchi zitakazoathiriwa zaidi na kuporomoka kwa uchumi wa dunia baada ya vita nchini Ukraine ni zile ambazo ni maskini, hivyo ni vema Wakazi wa mataifa tajiri kutotumia rasilimali zake kifahari na kuwakumbuka watu wasiokuwa na kitu.