Uchomaji mkaa wamuibua DC Nikki

0
123

Wakazi wa vijiji vya Lukenge, Magindu na Luzuguni wilayani Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kubadili mtazamo kuwa shughuli pekee itakayowapatia kipato ni kuchoma mkaa na badala yake wajikite kwenye shughuli nyingine kikiwemo kilimo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kibaha, Nickson Saimoni wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye vijiji hivyo, akifuatana na watumishi mbalimbali wakiwemo wa ofisi ya Mhifadhi Misitu mkoa wa Pwani.

Amesema ili kufanikisha jambo hilo, watendaji wa vijiji hivyo wanapaswa kushirikiana katika kutenga maeneo yatajayotumika kwa ajili ya kilimo.

Kwa upande wake Mhifadhi Mistu wilaya ya Kibaha, Mukama Kusaga amesema ukataji miti unaofanywa na wakazi wa vijiji
vya Lukenge, Magindu na Luzuguni umeharibu mazingira na kusababisha jangwa.

“Licha ya jitihada tunazofanya sisi TFS za kuwaelimisha wananchi kuachana na uvunaji holela wa misitu lakini wamekuwa si wepesi wa kuifikia hilo na badala yake wamekuwa wakijenga chuki na sisi jambo ambalo ni kinyume.” amesema Kusaga

Amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara wa mkaa hasa wanaosafirisha kwa kutumia pikipiki wamekuwa wakitumia njia zisizo rasmi kuwakwepa maafisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), jambo ambalo halikubaliki.