Uchaguzi Serikali za Mitaa kufanyika Novemba 24

0
236

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,  ametangaza  Novemba 24 mwaka huu kuwa siku ya  uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa  mikoa yote ya Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dodoma katika mkutano ulioshirikisha Wakuu wa Mikoa kutoka mikoa mbalimbali nchini, Watendaji  wa halmashauri na viongozi wa Vyama vya Siasa, Jafo amesema kuwa kanuni na miongozo kwa ajili ya uchaguzi huo zimekamilika.

Ameongeza kuwa, Watanzania wote wanatakiwa kujitokeza kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huo wa Serikali za Mitaa.

Waziri Jafo pia amewataka Watanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano wakati wote wa kujiandikisha, kampeni, kupiga kura na hata baada ya uchaguzi huo.