Uchaguzi mkuu kufanyika Oktoba 28

0
317

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza kuwa uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara utafanyika Oktoba 28 mwaka huu siku ya Jumatano.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuwa kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 26 hadi Oktoka 27 mwaka huu.

Kwa upande wa uteuzi wa wagombea wa kiti cha Urais na Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani, utafanyika Agosti 25 mwaka huu.