Jumuiya ya Maridhiano Tanzania imekabidhi Tuzo ya Heshima kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kuendelea kuimarisha hali ya amani na utulivu nchini.
Tuzo hiyo imepokelewa mkoani Mbeya na mkuu wa mkoa huo Juma Homera kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Akipokea tuzo hiyo Homera amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri, afya pamoja na miradi ya maji mkoani humo.
Aidha, viongozi wa dini wa mkoa wa Mbeya wamefanya maombi maalum kuliombea Taifa amani na mvua na kutoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.