Tuweke pembeni ubinafsi tuupende mkoa

0
240

Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Seleman Mzee amewataka viongozi na wananchi wa mkoa huo kutanguliza mbele maslahi ya mkoa, badala ya kujadili ukabila kwani wote ni Watanzania.

Meja Jenerali Mzee ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kuangazia mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, uliofanyika katika manispaa ya Musoma.

Amesema sasa ni wakati kwa mkoa wa Mara kupata kituo cha mabasi cha kisasa na hivyo kuwataka viongozi wa mkoa huo kuelekeza nguvu zao katika kutafuta eneo kwa ajili ya mradi huo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara pia amewasisitiza viongozi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha inakamilishwa kwa wakati, huku akieleza kusikitishwa na kuwepo kwa miradi isiyokamilika kwa wakati pasipo sababu za msingi.