“Serikali ya Mama Samia imeanzisha project [programu] inaitwa Building a Better Tomorrow, (Kujenga Kesho Bora). Huwezi kuijenga kesho bora kwa kutumia umri wa mzee Kabudi. Tunaijenga kesho bora kwa kutumia umri wa wadogo zetu.
Rais Samia ameanzisha hii programu na nataka nikwambie tumetoa matangazo kwa ajili ya kuwachukua vijana kuwapeleka kwenye mafunzo ya miezi minne bure, kupewa elimu juu ya kilimo biashara baada ya hapo tutawapatia ardhi isiyopungua hekari 10 katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu.”- Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe