Mkuu mpya wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian amesema anataka kuona huduma za afya zikiimarika ndani ya mkoa huo na vifo vya Wajawazito vinapungua.
Dkt. Burian ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watendaji wa Serikali mkoani Tanga mara baada ya kupokelewa mkoani humo ambapo pia amemuapisha mkuu mpya wa wilaya ya Mkinga, Kanali Evans Mtambi.