TUNAPATA TABU MIKOA ISIYO NA SHULE ZA UADILISHO

0
131

Dkt. Salma Fundi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ustawi wa Jamii amesema moja ya changamoto zinazohitaji ufumbuzi katika jamii ni ile ya kutokuwepo kwa shule za kutosha za uadilisho katika mikoa, jambo lililopelekea huduma hizo kuwa hafifu.

Dkt. Salma ameyasema hayo alipokuwa akitoa maoni wakati wa majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kiukweli tunapata tabu sana na hawa watoto ambao wanakuwa watukutu kuwaadilisha kwa sababu shule za kuwafundishia na kuwabadilisha ni chache, unakuta labda ipo Mbeya nyingine ipo Dar es Salaam mikoa mingine haina.
Sasa kwenye mikoa ambayo haina uadilisho wa watoto hawa inakuwa ni changamoto,”
amesema Dkt. Salma na kuongeza kuwa

” Lakini pia wamependekeza kuwepo na usimamizi wa wafungwa wa vifungo mbadala.. kweli na mimi nakubaliana nalo kabisa, hilo ni suala muhimu la ufuatiliaji wa maafisa ustawi wa jamii.”