Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Patrick Chandi, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuupatia mkoa wa Mara mradi wa reli utakaounganisha mkoa wa Mwanza na mji wa Musoma, Mara.
Chandi ametoa ombi hilo mkoani Mara wakati wa mkutano wa kuangazia miaka miwili ya mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.