Tunaomba barabara na umeme maeneo ya migodi

0
167

Mbunge wa Busanda mkoani Geita Mhandisi Tumaini Magesa, ameiomba Serikali kujenga miundombinu ya barabara na umeme kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini mkoani humo ili kurahisisha shughuli za uchimbaji madini na kuokoa gharama mbadala.

Magesa ameyasema hayo wakati wa ufungaji wa maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita na kuyataja maeneo yenye changamoto ya barabara na umeme ambayo ni barabara ya kutoka Buliyankuru – Kahama na Katoro – Magenge – Ushirimbo.

Ameongeza kuwa, kuwepo kwa changamoto hiyo ya barabara na umeme kunapelekea kutumia gharama nyingi katika kuendesha migodi hiyo na kusababisha wachimbaji wadogo kutokuwa na mazingira mazuri kushiriki kwenye shughuli za uchimbaji