Tumieni teknolojia kurahisisha kazi

0
299

Mwezeshaji wa mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) Dkt. Hilda Mwangakala amesisitiza walimu wa shule za sekondari kujikita zaidi katika matumizi sahihi ya teknolojia kwenye shughuli zao za kila siku ili kurahisisha kazi zote zinazomuhusu mwanafunzi.

Amesema matumizi ya teknolojia yanarahisisha kazi kwa kutumia muda mfupi zaidi tofauti na njia nyingine.

Dkt. Mwangakala ameyasema hayo mkoani Mwanza wakati wa
mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa shule za sekondari wa mikoa ya
Geita, Mara na Singida yanayofanyika katika Chuo cha Ualimu Butimba chini ya mradi wa
SEQUIP.

📸✍️ @e_j1official