Tumieni nishati mbadala
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahimiza Wananchi kutumia nishati mbadala na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kutunza mazingira.
Akizungumza katika Baraza la Eid Al Adha kitaifa kwenye msikiti wa Mohammed VI Kinondoni, Dar es Salaam Waziri Mkuu amesema, Serikali imeandaa mpango maalumu kuhusu matumizi ya nishati mbadala kama vile kuni na mkaa hasa kwenye taasisi zinazozidi watu 100 ambao kila siku wanatumia kuni na mkaa kuandaa chakula.
Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inakamilisha kutoa miongozo ya matumizi ya nishati mbadala na malengo ya Serikali kufikia Januari 2024 nishati mbadala ianze kutumika katika taasisi zote zenye watu zaidi ya 100 na kuendelea.