TUMEPELEKA TIMU HANANG KUIMARISHA MIUNDOMBINU

0
161

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema wizara yake imepeleka timu Katesh ili kuangalia uharibifu uliotokea kwenye miundombinu ya wizara hiyo kutokana na janga la mmomonyoka wa udongo kufuatia mvua kubwa zilizonyesha wilayani Hanang.

Akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam Waziri Nape amesema maagizo hayo ameyatoa kufuatia maelekezo aliyoyatoa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekeza nguvu ya Serikali wilayani Hanang kutokana na maafa hayo.

Nape amesema hadi sasa kwa taarifa alizopata miundombinu mingi ipo salama ila yapo maeneo machache ambayo miundombinu ya umeme imeharibika ambapo watoa huduma wametafuta njia mbadala kwa kuweka huduma ya dharura ya majenereta na huduma zimerejea kama awali.

Aidha, kwa maeneo ambayo miundombinu ya mawasiliano [fiber] imekatika juhudi za kuunganisha zinaendelea na kwa baadhi ya ofisi za posta zilizojaa matope zinasafishwa ili huduma iendelee kama awali.