Tume yabaini viongozi wa kisiasa kutumia dola kukamata watu

0
137

Tume ya kuboresha Mfumo na Taasisi za Haki Jinai nchini imebaini baadhi ya viongozi wa juu wa kisiasa kuingilia mnyororo wa haki jinai kwa kuamuru vyombo vya dola kukamata na kuwaweka ndani Wananchi wakati mamlaka hayo hawana.

Akisoma taarifa rasmi ya Tume hiyo leo Julai 15, 2023 Ikulu, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande amesema, Viongozi hao waelekezwe kuzingatia sheria ili waache jambo hilo.

“Tume imebaini kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa siasa wamekuwa wakitoa matamko na amri za kuamuru vyombo vya dola kukamata na kuwaweka ndani Wananchi wakati mamlaka hayo hawana, hivyo viongozi hao waelekezwe kuzingatia sheria.” Ameshauri
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande