Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema iko tayari kuendesha na kusimamia uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa wadau mbalimbali wilayani Babati mkoani Manyara Afisa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Upendo Mbwambo amesema tayari baadhi ya vifaa vitakavyotumia katika uchaguzi huo vimeshawasili na vingine viko katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.
Pia amesema katika uchaguzi wa mwaka huu zaidi ya wapiga kura 29,000 wamejiandikisha huku wanawake wakiwa zaidi ya asilimia 50.3.
Tume imewataka wanasiasa na wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu huku wakikumbuka sheria za nchi zipo na hakutakuwa na msamaha kwa kisingizio cha uchaguzi na kuwataka wananchi kujitokeza siku ya kupiga kura ili kutumia haki yao ya kuchagua viongozi watakao timiza matarajio yao.