Katika kupambana na ongezeko la wahitimu wa elimu ya juu kukosa ajira chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam Tudarco kimeandaaa kozi maalum za shahada za uzamili ya uongozi wa biashara na shahada za uzamili ya taaluma ya habari (masters) ili kuwawezesha wahitimu kujiajiri
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm Naibu mkuu wa chuo na taaluma Tudarco Profesa ANDREW MOLLEL amesema kozi hizo zitasaidia wahitimu kuweza kujiajiri badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya taaluma ya habari Dokta GETRUDE NTULO amesema fursa ya chuo cha tumaini itawezesha maafisa habari kuongeza ujuzi kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari.
Kozi ya shahada zitatolewa katika masomo ya jioni ambapo waombaji wenye shahada ya awali bachelor Degree yenye ufaulu wa wastani wa GPA 2.7 kutoka chuo chochote kinachotambulika wataruhusiwa kujiunga na kozi hizo.