Tuliyokubaliana SADC Yakitekelezwa Yataleta Manufaa Makubwa: Rais Dkt Magufuli

0
246
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. John Pombe Magufuli, wa pili kutoka kulia, Rais wa Namibia Hage Geingob na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kulia pamoja na marais wengine hawapo pichani wakipiga makofi mara baada ya kusaini makubaliano manne ya Itifaki kwa nchi za SADC, katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi na kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC,Dkt. Stergomena Tax

MWENYEKITI wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa agenda na maazimio yaliyopatikana kupitia mkutano huo yakitekelezwa kwa vitendo yataleta manufaa makubwa kwa nchi wanachama.


Akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amesema kuwa mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na wamefikia makubaliano katika masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza katika viwanda ili kufikia azma iliyowekwa 2015)2063 na hiyo ni pamoja na kuboresha mazingira,

kutoweka vikwazo katika mipaka, kupambana na ukiritimba katika maamuzi pamoja na kupambana na rushwa huku akieleza mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi ndani ya jumuiya hiyo.


Aidha katika mkutano huo wakuu wa nchi wamedhamiria kushirikiana katika kudumisha amani katika nchi ya Jamhuri ya Kongo pamoja na kuunda chombo maalumu chakupambana na majanga mbalimbali ikiwemo ukame, mafuriko, ukame na njaa chombo ambacho kitakuwa chini ya sekretariti ya jumuiya hiyo.


Vilevile Rais Magufuli amesema kuwa katika mkutano huo wamejadili hali ya uchumi katika ukanda wa jumuiya wanachama ambapo uchumi ulikua kwa asilimia 3.1 pekee tofauti na malengo waliyojiwekea ya kukuza uchumi kwa asilimia 7 hali iliyosababishwa na majanga katika baadhi ya nchi wanachama na wamekubaliana kuwekeza katika miundombinu pamoja na kuboresha uchumi wa fedha.


Hata hivyo kupitia mkutano huo wamejadili mapato yatokanayo na jumuiya hiyo ambapo nchi wanachama zimehimizwa kulipa ada zao pamoja na kuongeza mapato kwa kuangalia njia mbadala ya kuchangia na kwa niaba ya wanajumuiya hiyo Rais Magufuli amewashukuru washirika kwa kushirikiana nao ambao wamekuwa wakishirikiana na jumuiya hiyo na hao ni pamoja na umoja wa Ulaya (EU), Ujerumani, China, Sweden, benki ya dunia, Global fund, na benki ya Afrika kwa ushirikiano na michango yao.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli, wa pili kutoka kulia, Rais wa Namibia Hage Geingob (alieyemaliza muda wake wa Uenyekiti) kulia pamoja na marais wengine hawapo pichani wakisaini Itifaki nne walizokubaliana kwa nchi za SADC,  katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi na kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC,Dkt. Stergomena  Tax. 


Rais Magufuli ameahidi ushirikiano kwa muda huo wa mwaka mmoja wa uenyekiti watahakikisha jumuiya hiyo inapiga hatua zaidi hasa katika masuala ya viwanda na biashara ili kujenga uchumi imara kwa nchi wanachama.