Tulia Trust yatambua mchango wa TBC

0
136

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa cheti maalum kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Mbeya kwa kutambua mchango na ushiriki wa shirika hilo katika kutangaza tamasha la ngoma lililofanyika mwisho mwa mwaka 2021 jijini Mbeya.

Cheti hicho kimekabidhiwa
na Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust mkoani Mbeya Jackline Boaz
kwa mkuu wa TBC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Gift Ambwene.

Akipokea cheti hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Gift ameishukuru taasisi hiyo ya Tulia Trust na kuahidi shirika hilo litaendelea kushirikiana na taasisi hiyo.