Mtanzania yeyote anaruhusiwa kutembelea Bunge wakati vikao vya Bunge vikiendelea kwa lengo la kujifunza na kujionea utendaji kazi wa mhimili huo.
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari bungeni jijini Dodoma.
Amesema mwananchi anaweza kwenda bungeni kwa kualikwa na mbunge au kwa kuandika barua kuomba kufika bungeni.
Ameongeza kwamba mwananchi anapoandika barua anatakiwa kutaja tarehe ambayo angependa kufika bungeni, lengo likiwa ni kuratibu wageni wanaoomba kufika kwa siku husika.