Treni yapata ajali Kidete

0
219

Treni ya abiria imepata ajali katika eneo la Kidete lililopo mpakani mwa wilaya za Kilosa mkoani Morogoro na Mpwapwa mkoani Dodoma.

Habari kutoka mkoani Morogoro zinasema, kwa sasa Kamanda wa polisi wa mkoa huo akiwa ameongozana na maofisa wengine wanaelekea eneo ilipotokea ajali hiyo.

Taarifa za awali zinadai chanzo cha ajali hiyo ni gari kuigonga treni hiyo ya abiria.

Mpaka sasa bado haijfahamika madhara yaliyotokana na ajali hiyo.