TPDC yaendelea kusambaza gesi asilia majumbani

0
193

Wakazi takribani 506 wa Dar es Salaam wanatarajiwa kunufaika na mradi wa gesi asilia inayosambazwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambapo ni muendelezo wa utoaji wa huduma ya gesi asilia inayotumika majumbani, kwenye magari na viwandani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio mara baada ya kukagua uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya kulaza mabomba ya kusambaza gesi majumbani katika maeneo ya Sinza.

“Waziri wa nishati aliagiza kuangalia upya namna ya kurahisisha usambazaji wa gesi asilia kwa wananchi, nasi tumeamua kuwatumia wazalishaji wa ndani wa vifaa vya usambazaji wa gesi hiyo ambapo itapunguza muda kutoka mwaka mmoja tuliokuwa tunatarajia kukamilika hadi kufikia miezi sita,” ameongeza Dkt Mataragio.

Kwa upande wake mkandalasi wa ujenzi wa mradi huo Mhandishi John Bula amesema kwa kutumia wazalishaji vifaa vya kusambazia gesi wa ndani kumeokoa muda mwingi na gharama kuliko wangetumiwa na wazalishaji wa nje.