Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara (Mtwara Technical) imeanza rasmi kutumia gesi asilia kama chanzo cha nishati shuleni hapo.
Awali, shule hiyo ilikuwa ikitumia kuni ambazo zilisababisha ukataji wa miti kwa wingi na hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira.
Kwa upande mwingine, Gereza la Lilungu mkoani Mtwara lipo mbioni kuanza kutumia nishati hiyo baada ya ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia kuelekea gerezani hapo kukamilika.
Kukamilika kwa miundombinu hiyo kutasaidia kupunguza gharama za kuni pamoja na kuepusha uharibifu wa mazingira.
Pichani ni majiko ya Gesi asilia katika Shule ya Ufundi ya Mtwara mara baada ya kukamilika kwa mradi wa gesi asilia uliofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) shuleni hapo.